FM Manyara
FM Manyara
4 December 2025, 2:13 pm

Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara imetoa tuzo na zawadi kwa walimu na shule zilizofanya vizuri katika ufaulu wa masomo .
Na Angel Munua
Hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa ikiwa na lengo la kutoa hamasa kwa walimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao ambapo afisa elimu halmashauri ya wilaya ya Babati Simoni Mumbe amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanavyofanya na kuhakikisha ufaulu unaongezeka .
Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Babati mjini Emmanuel Kambai amewapongeza walimu kwa kuongeza ufaulu ambapo ameahidi kushirikiana vizuri na wadau waelimu ili kutengeneza maz ingira rafiki ya ufaulu kwa wanafunzi.

Aidha kwa upande wa walimu ambao wamepata tuzo na zawadi kwa kufanya vizuri katika masomo yao wameishukuru halmashauri hiyo kwa kuandaa jambo hilo kwani limewatia hamasa ya kuzidi kufundisha kwa bidii .