FM Manyara
FM Manyara
4 November 2025, 5:04 pm

Maafisa usafirishaji wilayani Babati mkoani Manyara wamelalamikia kuadimika kwa mafuta katika vituo vya kuuzia mafuta na kuiomba Serikali kuingilia kati suala hilo ili kurahisisha shughuli za uchumi kwa wananchi.
Na Marino Kawishe
Wakizungumza na fm Manyara wamesema, kituo kinachouza mafuta ni kimoja hali inayosababisha kuwepo kwa foleni ya kupata huduma hiyo, ambapo wanalazimika kupandisha bei ya nauli.
Kufuatia changamoto hiyo Fm Manyara imemtafuta katibu mkuu wa Latra CCC mkoani Manyara Claudina Haule amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakipandisha nauli kiholela wakati huu wa changamoto ya usafiri mkoani Manyara jambo ambalo ni kinyume na taratibu zilizowekwa na Mamlaka husika, amesema watachukua hatua za kisheria kwa madereva watakaobainika kwenda kinyume na sheria zilizowekwa na latra.