FM Manyara

Sillo ahitimisha kampeni Babati vijijini

28 October 2025, 9:46 am

Picha ya Mgombea Ubunge jimbo la Babati vijijini Danieli Sillo

Na Marino Kawishe

Kampeni za mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM jimbo la Babati Vijijini  zimehitimishwa rasmi octoba 27,2025 ambapo Zaidi ya wapiga kura laki mbili na elfu kumi na mbili wanatarajiwa kupiga kura katika jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Nchini October  29, 2025.

Akizungumza mbele ya wananchi na wajumbe  wa ccm kutoka maeneo mbali mbali ya jimbo la Babati Vijijini waliokutana katika kata ya kiru six, mgeni rasmi kwenye mkutano huo ambaye ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Manyara Jane’s  Darabe amesema wamenadi ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

Sauti ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Manyara

Aidha Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi jimbo hilo Daniel Baran Sillo amewaomba wananchi wa jimbo la Babati Vijijini kujitokeza kupiga kura kumchagua Rais Samia, wabunge pamoja na madiwani kutoka chama cha mapinduzi.

Sauti ya mgombea Ubunge Jimbo la Babati vijijini

Kwa upende wake mwenye-kiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini Jackson Haibei amesema wamefanya kampeni katika kata zote 25 zinazounda jimbo hilo na kilichobaki ni wananchi kufanya maamuzi kwenye sanduku la kura siku ya uchaguzi October 29.

Sauti ya mwenye-kiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini Jackson Haibei

Uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais, Wabunge na madiwani nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu 2025.