FM Manyara
FM Manyara
27 October 2025, 12:54 pm

Siku moja kabla yakufungwa kwa kampeni za Wagombea urais, wabunge na madiwani wananchi wa kata ya Secheda, Dabil na Madunga zilizopo katika jimbo la Babati Vijijini wametakiwa kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura hapo October 29.
Wito huo umetolewa na mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM jimbo la Babati Vijijini Daniel Baran Sillo wakati akiomba kura za ndio kwenye kata hizo.
Kwa upande wake mjumbe wa mkutano Mkuu taifa CCM Wilaya ya Babati Steven Manda amesema zipo sababu kwanini wananchi wapige kura kuchagua Mgombea kutoka CCM.
