FM Manyara
FM Manyara
27 October 2025, 12:01 pm

Watanzania kote Nchini wametakiwa kuendelea kuliombea taifa Wakati huu Nchi ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano maalumu wa maombi wakuliombea taifa uliofanyika katika kata ya Bashnet jimbo la Babati Vijijini mkoani Manyara Waziri mkuu Mstaafu Frederick Sumaye amesema umoja na ushirikiano miongoni mwa Watanzania unatakiwa bila kubagua kabila la mtu.
Kwa upande wake mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM jimbo la Babati Vijijini na naibu waziri wa Mambo ya ndani Daniel Baran Sillo amewata wananchi kuombea aman kabla ya uchaguzi wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi….
Mkutano huo maalumu wakuombea amani ya Nchi kabla ya uchaguzi umehudhuriwa na badhi ya viongozi wa kidini pamoja na mila kutoka simanjiro, kiteto, Hanang na Halmashauri ya Babati Vijijini.
