FM Manyara
FM Manyara
24 October 2025, 12:35 am

Zikiwa zimesalia siku tano kabla ya uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu hapa Nchini, Watanzania wamehimizwa kujitokeza na kupiga kura kwa wingi.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ayalagala Mratibu wa kampeni kwa Kanda ya Kaskazini Na waziri mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye amesema zipo ahadi ambazo zimetajwa na mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr Samia Suluhu Hassan ambazo zitafanyiwa kazi kwa siku mia moja iwapo atashinda.
Naye Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini Daniel Baran Sillo amesema vipaumbele vyake vyote alivyoahidi kwenye kampeni atavipa msukumo mkubwa kwasababu analo deni la kuwalipa wapiga kura wake.
Aidha Sillo amesema ni kweli hana mpinzani lakini hilo halitoshi kusema ameshinda lazima wananchi kujitokeza kupiga kura ya ndio ili aweze kushinda na kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
