FM Manyara
FM Manyara
22 October 2025, 10:58 pm

Wananchi wa kata ya magugu wametakiwa kujitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu kwani hakuna yeyote atakayefanya fujo bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwenye uchaguzi huo ambo umepangwa kufanyika October 29 mwaka huu.
Na Marino Kawishe
Akiwahutubia Wananchi wa kata hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya ndani Daniel Baran Sillo amesema serikali bado ipo kazini na watu wajitokeze kwenda kupiga kura na kumchagua Rais, Wabunge na madiwani kutoka CCM siku ya uchaguzi.
Aidha Mgombea huyo amesema iwapo Rais Samia ambaye ni mgombea urais kupitia chama chake cha CCM atapata Ridhaa ya Wananchi kwenye uchaguzi huo tayari Kuna mambo ambayo ameahidi kuyatatua kwa siku mia moja ikiwemo kuongeza ajira kwa kada ya afya pamoja na waalimu na kuongeza fedha kiasi cha sh Bilion 200 za mikopo.
Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya magugu Stanley Dismas amewataka wananchi kumchagua Kwa kura nyingi ili ashirikiane na mbunge kutatua kero mbali mbali zinazoikabili kata ya magugu ikiwemo bei ya umeme ambayo ni kubwa kwa wananchi wa kijijini hicho.
Aidha mwenyewe kiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini Jackson Haibei amesema Siku zilizosalia ni chache hivyo kila mwenye vigezo vya kupiga kura ajitokeze kuchagua Mgombea wa ccm.
Katika mkutano huo aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kata ya Nkaiti na wanachama wengineni kumi na tisa wa CHADEMA na Mmojaa kutoka Chama cha NCCR-Mageuzi wamejiunga na CCM leo kwenye mkutano huo.
Zimesalia siku saba pekee kabla ya Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kufanyika October 29 hapa nchini huku wagombea mbali mbali wakitumia siku hizo kujinadi kwa wananchi kuomba kuchaguliwa katika uchaguzi huo.
