FM Manyara
FM Manyara
21 October 2025, 11:13 pm

Na Marino Kawishe
Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini Danieli Baran Sillo ameendelea kunadi ilani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 29, kwa wananchi wa kata ya Magara na Mwada kwa kuhaidi kukamilisha miradi mbali mbali iliyoanzishwa kwa miaka mitano iliyopita.
Akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni Mgombea ubunge wa jimbo hilo Daniel Baran Sillo amesema tatizo la kutokuwepo kwa maji safi na salama pamoja na umeme kwa baadhi ya Vitongoji ameyapokea na atayafanyia kazi baada ya kupata ridhaa yakuchaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Nchini October 29.
Kwa upande wake Mgombea udiwan wa kata ya Magara Gonzalez Mkoma amemuomba Mgombea ubunge Wa Jimbo la Babati Vijijini kukamilisha changamoto hizo na kuomba wananchi kumchagua kwa kura ya ndio ili aweze kusaidiana na mbunge kukamilisha miradi hiyo.
Mgombea ubunge huyo anatarajia kuendelea na mikutano ya kampeni hapo kesho October 22 kwenye kata ya magugu na kiru.
