FM Manyara

Sillo awataka wananchi kujitokeza kupiga kura octoba 29

20 October 2025, 11:13 pm

Picha ya mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Daniel Baran Sillo akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Endabegi kilichopo kwnye kata ya Riroda

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, wananchi wa kata za Riroda na Duru wilayani Babati, mkoani Manyara, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kupiga kura na kuwachagua viongozi kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.

Na Marino Kawishe

Zikiwa zimesalia siku nane pekee kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao utafanyika oct 29 mwaka huu wiki ijayo wananchi wa kata ya Riroda na Duru wilayani Babati Mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kumchagua Rais, Wabunge na madiwani wa CCM.

Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Endabegi kilichopo kwenye kata ya Riroda  mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Daniel Baran Sillo amesema wananchi  wapige kura kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.

Sauti ya mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM

Kwa upande wake mwenyewe kiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini Jackson Haibey amesema jumla ya bilion 242 zimetekeleza miradi mbali mbali kwenye jimbo la Babati Vijijini kwasababu ya wananchi kuchagua CCM. 

Sauti ya mwenyewe kiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini

Nae mgombea udiwani ambaye hana mpinzani katika kata ya Riroda Nyangweli Bombo amewasilisha changamoto zinazoikabili kata hiyo nakuomba zitatuliwe mara baada ya uchaguzi…

Sauti ya mgombea udiwani wa kata ya Riroda

Mpaka sasa Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini amezifikia kata 23 na kubakiza kata mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa October 29.