FM Manyara
FM Manyara
17 October 2025, 8:02 pm

Na Marino Kawishe
Mgombea ubunge wa jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini Daniel Baran Sillo ameendelea na ziara ya kunadi ilani ya chama cha mapinduzi CCM nakuomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya October 29 mwaka huu kupiga kura na kumchagua Rais, Mbunge na Madiwani wa chama hicho.
Sillo amesema hayo leo katika mikutano ya hadhara ya kampeni kwenye vijiji vya Manyara na Ayamango vilivyopo katika Kata ya Galapo Wilayani Babati mkoani Manyara.
Aidha amesema iwapo atachaguliwa kwa kura za ndio kwenye uchaguzi huo ahadi zote zilizoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama hicho kwenye jimbo hilo atahakikisha zinatekelezwa ili kulipa deni kwa Wananchi waliopiga kura.
Mkutano huo wa hadhara pia umehudhuriwa na mwenyekiti wa ccm Wilayani Babati ndugu Jackson Haibey pamoja na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi wilaya Agatha Rafael na wajumbe wengine wa ccm kutoka kata na vijiji vya Galapo.
Mgombea huyo wa Ubunge kwa jimbo la Babati Vijijini mpaka sasa ameshazifikia kata 19 na kubakiza kata sita kati ya kata 25 za jimbo la Babati Vijijini.
