FM Manyara
FM Manyara
9 October 2025, 9:48 pm

Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kuongeza thamani ya mazao ya mbogamboga na mikunde kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao hayo ili kupata masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi badala ya kuuza mazao ghafi kwa bei ya chini.
Na Mzialfa Zaid
Akizungumza katika mafunzo ya kuongeza thamani ya mazao ya mbogamboga na mikunde yaliyoandaliwa na Shirika la World Vegetable Center kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na Sido, Kaim Katibu tawala mkoa wa Manyara Faraja Ngerageza amesema itasaidia kuongeza thamani ya mazao yanayopatikana ndani ya mkoa wa Manyara.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi wa kitengo cha uchumi jamii kutoka Shirika la World Vegetable Center Inviolate Dominick amesema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wakulima wanaotengeneza bidhaa mbali mbali kutokana na mboga mboga na mikunde.

Meneja wa Sido mkoa wa Manyara Abel Mapunda amewataka wananchi mkoani Manyara kufika Sido ili wajifunze ujasiriamali tofauti utakaowasaidia kuwainua kiuchumi.

Afisa biashara wa mkoa wa manyara Ally Mokiwa amesema mafunzo hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuinua kipato chao kupitia ubunifu.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kiuchumi kuongezewa thamani.
