FM Manyara

Dk. Samia atoa tamko sakata bei ya mbaazi kushuka

3 October 2025, 6:28 pm

Picha ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea na mazungumzo na serikali ya India katika kuhakikisha Bei ya mbaazi inapanda Ili wakulima wa mbaazi wanufaike na zao hilo.

Na Mzidalfa Zaid

Dokta Samia amesema hayo Leo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara baada ya kuanza kampeini zake rasmi katika mkoa wa Manyara, amewataka wananchi waendelee kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na mazungumzo.

Sauti ya Dokta Samia

Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Hanang Asia halamgha, amemshukuru Dokta Samia Kwa kuleta maendeleo katika wilaya ya Hanang katika sekta ya maji,umeme,barabara pamoja na elimu na kuwaomba wananchi kumchagua Kiongozi huyo.

Sauti ya Mgombea ubunge Asia Halamgha

Aidha, Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema wananchi wa Hanang wamejupanga kumpigia kura Kiongozi huyo kutokana na kazi kubwa ya maendeleo aliyoifanya katikati kipindi chote Cha uongozi wake.

Sauti ya Waziri mstaaafu Sumaye

Dokta Samia Suluhu Hassan kesho October 4 atazungumza na wananchi wa mkoa wa Manyara katika viwanja vya stendi ya zamani na kunadi sera zake.