FM Manyara

Kesi ya Chadema yaahirishwa Manyara

2 October 2025, 8:57 pm

Picha ya Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika katikati mwenye shuka jekundu kushoto kwake ni wakili Samwel Welwel na kulia kwake ni wakili Tadey Lister

Mahakama kuu Tanzania kanda ya Manyara chini ya jaji Nenelwa Mwihambi  imeahirisha bila kupanga tarehe kesi  iliyofunguliwa na  CHADEMA  dhidi ya msajili wa vyama vya siasa kupinga maamuzi yake ya kutowatambua viongozi walioteuliwa na baraza kuu januari 22, mwaka huu pamoja na kuzuia ruzuku kwa chama hicho.

kisi hiyo namba 23267/2025 imewakilishwa na mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili mkuu wa serikali Mark Mulwambo akisaidiwa na wakili Erigh Rumisha pamoja na wakili Nickson Tenges na mawakili upande wa chadema ni wakili Mpare Mpoki akisaidiwa na wakili Samwel Welwel pamoja na wakili Tadey Lister.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo mmoja wa mawakili wanaosimamia kesi hiyo  wakili Tadey Lister amesema  uamuzi huo umetolewa ili kupisha mahakama ya rufaa kutoa maamuzi ya rufaa iliyokatwa na upande wa serikali kupinga maamuzi madogo yaliyotolewa mahakamani hapo agost 28, 2025 na jaji wa mahakama hiyo Devotha Kamzora.

Sauti ya wakili Tadey Lister

Kwa upande wake katibu mkuu wa Chadema  John Mnyika amesema kufuatia maamuzi yaliyotolewa leo na mahakama kuu kanda ya manyara maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa hayatotekelezwa na kufanyiwa kazi na anapaswa kuingiza katika akaunti  ruzuku ya chama  kuanzia alipositisha mpaka sasa.

Sauti ya katibu mkuu wa Chadema  John Mnyika