FM Manyara
FM Manyara
30 September 2025, 7:16 pm

Na Marino Kawishe
Wazazi na Walezi wamehimizwa kutokuchoka kujinyima na kuwekeza kwa watoto wao ili wapate elimu bora itakayowasaidia kuchangamkia fursa mbali mbali wanapokuwa wamehitimu mafunzo yao.
Akizungumza na wananchi mkoani Manyara kwenye mahafali ya kumi ya shule ya Amka Africa Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa hapa nchini Wolter Kirita amesema kwa ulimwengu wa sasa zawadi kubwa itakayomsaidia mwanafunzi kwenye maisha yake ni elimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shule za Amka Africa na Angaza Manyara zilizopo mjini Babati Simon Msangi amesema wanafurahi kuona wazazi wanaendeleza ushirikiano baina yao na waalimu na sasa wameanza kufundisha somo la Kichina shuleni hapo somo ambalo linapendwa zaidi na wanafunzi.
Aidha uongozi wa shule hizo umekiri ongezeko la wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ambapo sasa wana zaidi ya wanafunzi elfu moja na mia nne, na kutoa fursa ya kuanza upanuzi wa miundo mbinu ya madarasa mapya.
Na katika kuunga mkono hilo mfanyabiashara maarufu mjini babati maarufu Mama Hango amechangia kiasi cha sh milion moja ili kuwezesha mipango hiyo kukamilika.
