FM Manyara
FM Manyara
25 September 2025, 9:45 am

Na Marino Kawishe
Kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika October 29 mwaka huu hapa Nchini Wananchi wa kata ya Riroda wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura wakiwa na kadi za mpiga kura ili kumchagua Rais Samia Suluhu Hasan.
Akifungua kampeni za mgombea Udiwani wa kata ya Riroda kwa tiketi ya CCM mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Regina Ndege amesema uchaguzi ujao ni muhimu kwa Wananchi na hasa kumchagua mgombea Udiwani huyo ambaye ataziwasilisha kero mbali mbali za wananchi wa kata hiyo kwa mbunge ili zitatuliwe.
Kwa upande wake mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara Janes Darabe amewataka wananchi kutumia kura yao kwa Rais Dr Samia Suluhu, Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini na Kwa diwani kwa kumpa kura ya ndio.
Aidha mgombea Udiwani wa kata ya Riroda Nyangweli Bombo amesema akichaguliwa kwa kura za ndio kwenye uchaguzi huo atahakikisha kijiji cha Sangara kinajengwa Zahanati itakayotumika kutoa huduma za afya kwa Wananchi wa Kijiji hicho.
