FM Manyara
FM Manyara
21 September 2025, 3:32 pm

Wazazi mkoani Manyara wametakiwa kuwalinda watoto wao ambao wamehitimu darasa la saba katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa kuingia kidato cha kwanza ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo huo umetolewa na mkuu wa shule ya Greenland Primary School inayopatikana wilayani Babati mkoani Manyara Hawa Ng’aida katika mahafali ya nne ya darasa la saba, amesema kumekuwa kukifanyika vitendo vya ukatili katika maeneo mbalimbali hivyo wazazi wanapaswa kuwalinda watoto hao ambao wamehitimu.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mwakilishi wa wahitimu wa shule ya Greenland Primary School Akram Hamis amesema shule imefanikiwa kuwa bora kila mwaka kwa kufaulu vizuri mitihani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Delphine Mselle amesema shule ina mazingira mazuri ya kufundishia ambapo amewataka wananchi kuwapeleka wanafunzi shuleni hapo ili wapate elimu bora huku akisema wanampango wa kuanzisha shule ya sekondari.
Aidha mgeni rasmi wa mahafali hayo ambae ni Mkurugenzi wa Shirika la COSTO Elianchea Shng’a amesema amefurahishwa na mindombinu ya shule hiyo na kuwahasa wazazi kutumia shule hiyo kukuza elimu ya watoto.