FM Manyara
FM Manyara
16 September 2025, 4:36 pm

Na Marino Kawishe
Wananchi katika jimbo la hanang mkoani manyara wametakiwa kujitokeza october 29 kwenye uchaguzi mkuu wakumchagua rais, wabunge na madiwani.
Akifungua kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la hanang kwa tiketi ya ccm, mjumbe wa mkutano mkuu taifa ccm Namelock Sokoine, amesema haoni sababu ya wananchi kushindwa kujitokeza kumchagua rais dkt Samia na Asia Halamga kama mbunge wao kwa kuwa mambo mengi yamefanywa Hanang kwa miaka 4 ya uongozi wa Rais dkt samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake mbunge anayewania ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya ccm Asia Halamga amesema vipaumbele vyake muhimu ambavyo atavisemea bungeni iwapo atapata ridhaa ya wana-hanang october 29 kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Katika ufunguzi huo wa kampeni katika jimbo la uchaguzi la Hanang umehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ambaye amesema wananchi wanapaswa kutumia tarehe ya uchaguzi kumchagua rais dkt Samia Suluhu Hasan, mbunge na madiwani wote 33 katika jimbo hilo.
