FM Manyara
FM Manyara
15 September 2025, 6:29 pm

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Babati CPA. Shaaban Mpendu amekabidhi vishikwambi kwa wataalam wa mifugo na kuwaasa kutunza na kutumia vishikwambi hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Na Mzidalfa Zaid
Amesema vishikwambi hivyo vimetolewa na serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi, ambapo jumla ya vishikwambi 12 vimetolewa ili kuongeza ufanisi na kuwezesha utoaji wa taarifa ya chanjo na utambuzi pamoja na kuingiza taarifa kwenye mfumo wa utambuzi na usajili katika zoezi la chanjo linaloendelea kitaifa.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo na mratibu wa chanjo halmashauri ya mji wa Babati Fatuma Mkombozi amesema hadi sasa wamefikia 62% ya uchanjaji kwa ng’ombe, 89% upande wa kuku, na 33.7% kwa mbuzi na kondoo.
Nao baadhi ya maafisa mifugo wa kata mbalibali za halmashauri ya mji wa Babati ambao wamekabidhiwa vishikwambi hivyo, wamesema vitawasaidia kurahisha utendaji kazi.

Aidha, zoezi la chanjo kwa mifugo lilianza tarehe 24 julai 2025 kwa upande wa kuku na agosti 20 2025 kwa ng’ombe,mbuzi na kondoo.