FM Manyara

Wafanyabiashara watakiwa kuwekeza Manyara

3 September 2025, 7:09 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga akiongea na wadau mbalimbali wa Biashara

Wafanyabiashara mkoani Manyara wametakiwa kuwekeza katika mkoa huo kwa kujenga hotel za kisasa, migahawa na nyumba za kulala wageni kutokana na kasi ya ukuaji wa mkoa.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akifungua Baraza la kumi na moja la wafanya biashara mkoa wa Manyara.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Manyara Mussa Msuya, amesema yeye pamoja na wafanyabiashara wengine wameanza kuwekeza kwa kujenga hotel, huku akiiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Sauti ya Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Manyara Mussa Msuya

Aidha, katika kikao hicho kumehudhuriwa na wadau mbali mbali mbali ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) ambapo mwakilishi wa Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya Kaskazini Arthur Lyatuu, amesema EWURA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo utatuzi wa migogoro inayotokea katika sekta ya maji, umeme na gesi.

sauti ya mwakilishi wa Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini