FM Manyara
FM Manyara
2 September 2025, 12:04 pm

Madaktari kutoka hospitali ya wilaya ya Babati kwa kushirikiana na shirika la So They Can Tanzania yaweka kambi ya siku sita kuhudumia wananchi wa kata nne za wilaya ya Babati.
Na Marino Kawishe
Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wamejitokeza kwenye siku ya kwanza ya kambi ya matibabu ya Afya iliyoandaliwa na shirika la So They Can Tanzania kwa ushirikiano na hospital ya Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara zoezi ambalo litadumu kwa siku sita kuanzia septemba mosi hadi septemba 6 mwaka 2025.
Akizungumza na Fm Manyara Radio meneja mkazi wa shirika hilo Roselyne Mariki amesema kambi hiyo ya siku sita itahudumia wananchi mbali mbali katika maeneo ambayo wamekuwa wakitoa huduma za elimu katika kata ya Galapo, Mamire, Qash na Endakiso.
Aidha huu ni mwendelezo wa shirika hilo lisilo la kiserikali kuendesha kambi za matibabu kwa wananchi mbali mbali wilayani Babati mkoani Manyara kwa lengo lakusaidia wananchi wenye hali ya chini ambapo siku ya kwanza ya utoaji huduma za afya ilikuwa katika shule ya msingi oimu iliyopo kata ya Galapo zaidi ya wananchi 350 wamejitokeza kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali nakupatiwa matibabu na madaktari kutoka hospital ya wilaya ya babati.