FM Manyara

Wazee Chadema waomba Lissu kuachiliwa huru

1 September 2025, 11:46 pm

Picha ya Mwenyekiti wa BAZECHA kanda ya Kaskazini Leonard Mao

Ili uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 uwe wa huru na haki chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetoa mapendekezo ya Ibara za katiba zinazotakiwa kufanyiwa maboresho.

Na George Augustino

Baraza Kuu la Wazee wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kaskazini (BAZECHA) wameeleza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yanayohitajika na chama hicho ili kuruhusu uchaguzi huru na wa haki. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama hicho Mkoa wa Manyara Mwenyekiti wa BAZECHA kanda ya kaskazini Leonard Mao amesema Chadema inahitaji mabadiliko na maboresho ya Katiba na Sheria ikiwa ni pamoja na kuwepo mgombea binafsi na mgombea huru wa nafasi za uongozi wa juu na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo haichaguliwi na Rais. 

Sauti ya Mwnyekiti wa BAZECHA Kanda ya Kaskazini

 

Aidha amesema baraza la wazee chadema lina laani kukamatwa na kuwekwa gerezani kwa Mwenyekiti wa chama chao Tundu lissu kwa madai yasiyo na msingi na kuomba Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) na mamlaka husika kumuachia huru Lissu bila masharti yeyote . 

Sauti ya Mwnyekiti wa BAZECHA Kanda ya Kaskazini