FM Manyara
FM Manyara
1 September 2025, 4:18 pm

Wawekezaji mkoani Manyara wanaohitaji kufuga wanyamapori na kuwapa fursa wananchi kuona wanyama katika maeneo yao, wametakiwa kuwasiliana na uongozi wa pori la akiba Mkungunero ili kupewa utaratibu wa kufuga wanyama hao.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezewa leo na afisa Utalii pori la akiba Mkungunero Wilfred Kilonzo wakati akiongea na Fm Manyara, amesema wanatoa fursa kwa wananchi kujiinua kiuchumi kupitia pori hilo kwa kuwafuga wanyama wanaoishi katika hifadhi kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake Afisa Mhifadhi Pori la akiba Mkungunero Tumain Minja, amesema kumekuwepo na changamoto ya wanyama kuvamia makazi ya watu, ambapo amewataka wananchi kutumia njia zinazotolewa na wataalamu kudhibiti wanyama hao wakiwemo tembo.