FM Manyara

Juma la elimu ya watu wazima kuadhimishwa Manyara September 2

29 August 2025, 6:07 pm

Picha ya waatalam wa elimu ya watu wazima

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kiujitokeza katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima linalotarajia kuanza september 2 hadi september 4 mwaka huu katika viwanja vya Stendi ya zamani.

Na Mzidalfa Zaid

Afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Manyara Ibrahim Mbogo, amesema  katika maadhimisho hayo kutakuwa na mafunzo ya utengenezaji wa vitu tofauti vitokanavyo na mazao au chakula kinachopatikana katika mkoa wa Manyara.

Sauti Afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Manyara Ibrahim Mbogo

Kwa upande wake Mkufunzi mkazi Taasisi ya elimu ya watu wazima Emanuel Geydan, amesema kutakuwa na banda la Taasisi ya elimu ya watu wazima ambapo kutatolewa elimu juu ya mtu mzima anaetaka kujiendeleza kielimu .

Sauti ya Mkufunzi mkazi Taasisi ya elimu ya watu wazima Emanuel Geydan

Aidha, amesema wanatoa elimu kuanzia ngazi ya chini ikiwemo elimu ya msingi na watu wazima wasiojua kusoma na kuandika , elimu ya sekondari kwa walioshIndwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbali mbali.