FM Manyara
FM Manyara
17 August 2025, 10:21 am

Vijana Wilayani Babati Mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia afya zao kwa kula vyakula ambavyo vina virutubisho ili kujenga na kulinda afya zao pia kupima afya zao mara kwamara na kujikinga na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya zinaa.
Na George Augustino
Halmashauri ya mji wa Babati kwakushirikiana na Shirika la Marie Stopes Tanzania wameandaa tamasha la vijana na kutoa elimu ya Afya ya uzazi na uzazi wa mpango, elimu ya lishe, ukatili wa kijinsia na elimu ya ujasiriamali kwa vijana na wananchi wa mji wa babati.
Akizungumza na fm manyara Mratibu wa miradi na masuala ya vijana kutoka Shirika la Marie Stopes Tanzania Tuponege Donald amesema wameitikia wito wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa babati kupitia ofisi ya mganga mkuu wa hospitali ya mji wa Babati kuja kutoa elimu kwa vijana jinsi ya kujikinga na kuepukana na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizotarajiwa.
Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa huduma ya Uzazi na mtoto katika Halmashauri ya mji wa Babati Restuta Massay amesema pamoja na elimu iliyotilewa katika tamasha hilo lakini pia huduma nyingine za afya zimetolewa ikiwemo uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi, upimaji wa virusi vya Ukimwi, presha, uzito pamoja na uchangiani wa hiyari wa Damu.
Tamasha hilo limefanyika katika uwanja wa Motel Papaa uliopo mjini Babati mkoani Manyara ambapo vijana pamoja na wananchi wa mji wa babati wamepata fursa ya kupata elimu hiyo ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango, elimu ya ukatili wa kijinsia pamoja na elimu ya ujasiriamali.