FM Manyara

RC Sendiga azitaka NGOs kujikita kusaidia jamii 

22 July 2025, 11:37 pm

Picha ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Manyara yametakiwa kujikita katika shughuli za kuisaidia jamii kwa kutatua changamoto zinazoikabili jamii hususani katika masuala ya lishe bora.

Na Angel Munuo

Wito huo umetolewa  leo na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akifungua kikao cha jukwaa la mashirika yasiyo yakiserikali kwa mkoa wa Manyara (NGOs) ambapo amesema  serikali imeweka mazingira rafiki na wezeshi kwa mashirika hayo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Kwa upande wake mkuu wa mashirika yasiyo ya kiserikali Patrick Gwasam amesema ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ngos ni makubwa na changamoto hizo ni masuala ya kikodi  ambayo wanapambana kuyatatua ili kuyasaidia mashirika ambayo yanachangamoto za kifedha katika kutekeleza majukumu yao ya kuisaidia jamii .

Sauti ya mkuu wa mashirika yasiyo ya kiserikali Patrick Gwasam

Nae afisa maendeleo ya jamii kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa manyara Anna Fisso ameelezea hali ya ukatili ilivyo kwa mkoa wa manyara.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii Anna Fisso