FM Manyara
FM Manyara
5 June 2025, 7:00 pm

Na George Augustino.
kijana aliyefahamika kwa jina moja maarufu la digidigi (48) amefariki dunia katika ajali ya gari la mizigo iliyotokea leo majira ya saa tano asubuhi katika daraja linalounganisha kijiji cha orongadida na kijiji cha majengo vilivyopo katika kata ya qash wilayani babati mkoani manyara .
akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mwenyekiti wa kijiji cha majengo saruni meliari amesema ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo lililokuwa limebeba mizigo ya wafanyabiashara wa mnada kutokea kijiji cha gallapo kufeli breki na kuangukiw katika korongo hilo na kumuua dereva aliyekuwa akiliendesha gari hilo.
kwa upande wao wananchi na wafanyabiashara waliokuwa wakisafiri na gari hilo wameiomba serikali kuwasaidia kurekebisha na kujenga upya daraja hilo ambalo limekuwa likisababisha vifo vya watu wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa.