FM Manyara
FM Manyara
5 June 2025, 6:32 pm

Kila tarehe 5 Juni, kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimazingira ikiwemo usafi wa mazingira na upandaji wa miti.
Na George Augustino
shirika lisilo la serikali la civil social protection lililopo wilayani babati mkoani manyara limeadhimisha siku ya mazingira duniani leo kwa kufanya usafi katika maeneo ya shule ya msingi darajani na katika eneo la mtaa wa maisaka b mjini babati mkoani manyara.
akizungumza na fm manyara wakati wa zoezi hilo afisa programu upande wa mazingira wa shirika hilo eliakim warikoi amesema wameamua kuadhimisha siku hii ili kuihamasisha jamii kuendelea kufanya usafi na kutunza mazingira pamoja na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira katika jamii na taasisi mbalimbali.
kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mtaa wa maisaka b wamesema wamehamasika kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira pamoja na shirika hillo katika mtaa wao kwakuwa usafi wa mazingira ni muhimu kwaajili ya kulinda afya zao kutokana na magonjwa ya mlipuko.
Aidha,mwalimu wa mazingira pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi darajani wamelishukuru shirika hilo la ulinzi wa jamii kwa kuwapa elimu ya utunzaji wa mazingira nakusema elimu hiyo wataitumia hata watakapokuwa majumbani.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira mwaka huu 2025 kitaifa ni “Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala”