FM Manyara

Halmashauri ya mji wa Babati yaazimia kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia

29 May 2025, 11:53 pm

Picha ya Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa babati Shaaban Mpendu

Ili kupunguza na kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara imejiwekea mikakati na kuamua kutekeleza maazimio ya kupambanana ukatili wa kijinsia

Na George Augustino

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu amewaagiza viongozi na watendaji wote wa vijiji, mitaa, kata na tarafa kufanya vikao kazi kwa kuwaalika wataalamu wa halmashauri pamoja na viongozi wa madawati ya kijinsia  kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto.

Mpendu ametoa agizo hilo leo katika kikao kazi cha cha kujadili na kutekeleza maazimio ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya mji wa Babati kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo kilichohusisha wadau mbalimbali yakiwemo mashirika binafsi .

Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati

Akitoa taarifa ya hali ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya mji wa Babati afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri hiyo Damian Nyamaka amesema mwaka 2022 halmashauri ilikuwa na jumla ya kesi 683 mwaka 2023 kesi 1,761 mwaka 2024 kesi 1,220 na mwaka huu 2025 hadi kufikia mwezi wa nne kumekuwa na kesi 416.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi kutoka kitengo cha dawati la jinsia na watoto wilaya ya Babati Bi Fatuma amesema kwa kipindi cha January hadi march mwaka huu 2025 jumla ya matukio ya ukatili yaliyoripotiwa ni 68 ambapo kati ya hayo 36 yalijumuisha umri wa chini ya miaka 18 na 32 yalihusisha watu wazima .

Sauti ya mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia wilaya ya Babati

Nao baadhi ya wadau waliochangia mjadala katika kikao hicho wameomba marekebisho ya sheria ya ndoa yafanyike haraka ili kuondoka na na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na watoto.

Sauti za wadau wa maendeleo ya jamii