FM Manyara
FM Manyara
14 May 2025, 8:11 pm

Jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Manyara limefanyika leo, ambapo mkuu wa mkoa wa Manyara Qqueen Sendiga, amewataka wananchi kujiunga na vyama vya ushirika ili kunufaika na fursa zinazopatikana ndani ya vyama hivyo.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka viongozi wa vyama vya ushirika mkoani hapa kuhakikisha wanasimamia sheria,miongozo na kanuni zilizowekwa ili vyama hivyo viendelee kukua.
Ametoa wito huo leo katika jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Manyara, amesema vyama vya ushirika vina mchango mkubwa ndani ya mkoa, hivyo viongozi wanapaswa kutatua migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza .
Kwa upande wake mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Absalom Cheliga amesema vyama vya ushirika vimekuwa vikifanya kazi kuhakikisha vinawainua wanaushirika huku akisema mkoa wa Manyara una jumla ya vyama 118 ambavyo vimesajiliwa na wanachama 11,517 wamesajiliwa.
Nae mwenyekiti wa jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika Yuda Sulley , amesema mfumo wa stakabadhi ghalani endapo utasimamiwa vizuri utasaidia kuwakomboa wakulima huku akisema kauli mbinu ya mwaka huu ni (ushirika hujenga ulimwengu ulio bora).
