FM Manyara

Wakulima Manyara tumieni mbegu za asili

7 May 2025, 5:27 pm

picha ya mbegu za asili

Wakulimà mkoani Manyara watakiwa kuendelea kuzalisha mbegu za asili na kuzitumia kwa matumizi ya chakula na biashara ili zisitoweke kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi. 

Na Angel Munuo

Wakulimà mkoani Manyara  wametakiwa kulima kwa kutumia mbegu za asili za mazao mbali mbali kwaajili ya chakula ,biashara na kuendelea kuzitunza zisitoweke kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi. 

Wito huo imetolewa na William Hamis kutoka kitengo cha Taifa cha vinasaba vya mimea kwa kushirikiana na shirika la DMDD kanisa katoliki jimbo la mbulu alipokuwa akizungumza na wakulimà wadogo nakuwataka wakulimà kuendelea kuzalisha mbegu za asili na kuzitumia kwa matumizi ya chakula.

sauti ya William Hamis kutoka kitengo cha Taifa cha vinasaba vya mimea

Baadhi ya wakulima wamesema elimu hiyo itawasaidia kwakua walikua wameshaacha kuzitumia mbegu za asili katika kilimo na matumizi ya chakula kwa kuona zimepitwa na muda nakusema  elimu hiyo imewasaidia kujua faida ya mbegu za mazao ya asili.

Aidha mnufaika wa kilimo cha mbegu za asili kutoka wilaya ya karatu mkoani Arusha amesema katika vikundi walivyo anzisha wamefanikiwa kukusanya  baadhi ya mbegu za asili  na kuzizalisha na nyingine ili kuzihifadhi katika benki ya mbengu ili kuzitunza zisitoweke.

sauti ya mnufaika