FM Manyara
FM Manyara
6 May 2025, 5:31 pm

Mkurugenzi mkaazi wa shirika la So They Can Tanzania (STC) amesema kipaumbele cha mradi unaotekelezwa na shirika hilo ni uboreshaji wa madarasa, majiko banifu pamoja na ujenzi wa vyoo vipya kwenye shule za msingi na sekondari.
Na Marino Kwishe
Zaidi ya Bilioni moja na milion mia nane za kitanzania zimetengwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la So They Can Tanzania (STC) kwaajili ya mpango wa kuboresha elimu kwenye kata nne za miradi ya shirika hilo ambazo ni Galapo, Qash, Endakiso pamoja na Mamire zilizopo halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Akitoa repoti ya utekelezaji miradi mbali mbali iliyokamilika na inayoendelea kujengwa mbele ya Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo, Mkurugenzi mkaazi wa shirika hilo Roselyne Mariki amesema kipaumbele cha Mradi huo ni uboreshaji wa madarasa, majiko banifu pamoja na ujenzi wa vyoo vipya kwenye shule za msingi na Sekondari.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo amewataka Wananchi wa maeneo ambayo yanapitiwa na Miradi hiyo kuendelea kushirikiana na wawekezaji hao ili kuitunza miundombinu iliyojengwa kwa Gharama kubwa pamoja na nguvu za wananchi ambazo zimesaidia kukamilika kwa miundombinu hiyo.
Nae Afisa elimu kata ya Endakiso Melkiory Gobre amewahimiza Wananchi wa kata za miradi ya STC kupeleka watoto wao shule kwakua hakuna kisingizio cha ukosefu wa Madarasa.
Aidha,Miradi ambayo imekamilika ni pamoja na Madarasa, Vyoo, majiko banifu na mabweni mbali mbali yaliyojengwa kwenye shule za msingi na sekondari kwenye kata zote nne.