FM Manyara

Sumu kuvu ilivyoathiri watoto Babati

26 March 2025, 7:47 pm

Imeelezwa kuwa baadhi ya watoto wa kuanzia umri wa miezi 6- 24 wilayani Babati mkoani Manyara wameathiriwa na changamoto ya sumu kuvu kutokana na jamii kutokuwa na uelewa wa kuhifadhi mazao katika sehemu salama.

Na Mzidalfa Zaid

Kufuatia utafiti uliofanyika wilayani Babati mkoani Manyara asilimia 70 ya watoto wamekutwa wameathiriwa na sumu kuvu itokanayo na vyakula wanavyovitumia, ambapo wazazi na walezi mkoani Manyara wametakiwa kuandaa vyakula bora ili kuwalinda watoto.

Hayo yameelezwa leo na Naeliwa Mshanga ambaye ni mwanafunzi wa uzamivu NMAIST katika semina iliyoandaliwa na shirika la Oikos East Africa na kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanawake  wanaonyonyesha, maafisa  lishe, maafisa kilimo, mganga mkuu, wawakilishi kutoka Imperial uUniversity, Leeds University na Nelson Mandela University.

 Amesema kwa utafiti ambao ulifanyika mwaka 2022 umebaini kuwa hali ya sumu kuvu katika wilaya ya Babati ni asilimia 70 na kupelekea kuwepo kwa udumavu ukiwa na asilimia 32, kilo pungufu asilimia 20 na ukondefu asilimia 4.

Sauti ya Naeliwa Mshanga ambae ni mwanafunzi wa uzamivu NMAIST

Kufuatia tafiti hizo afisa kilimo mkoa wa Manyara Paulo Eugene, amewataka wakulima kukausha na kuhifadhi  vizuri mazao Ili kudhibiti sumu kuvu kuingia kwenye mazao.

Sauti ya afisa kilimo mkoa wa Manyara Paulo Eugene,

Naye mwakilishi wa mganga Mkuu wa Wilaya ya Babati Jacobo Mwanamtwa amewataka wazazi na walezi kupanga utaratibu wa vyakula kulingana na umri wa watoto ambapo amesema wanaendela kutoa elimu hiyo Kila kijijji juu ya umuhimu wa lishe Bora Kwa watoto.

Sauti ya mwakilishi wa mganga mkuu wa wilaya ya BabatiJacobo Mwanamtwa

Aidha , Dr Monica Pirani ni  mtafiti mkuu wa chuo kikuu Cha Imperial university London amesema hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti tatizo Hilo ni pamoja na kuongeza elimu ya lishe Ili kuhamasisha jamii kupambana na utapiamlo pamoja na kuimarisha huduma za afya Ili kufikia vijiji vya mbali zaidi.

Sauti ya Dr Monica Pirani ambae ni  mtafiti mkuu wa chuo kikuu Cha empirio London

Nao baadhi ya wanawake wanaonyonyesha ambao wameshiriki katika semina hiyo, wamewashukuru waandaaji wa semina hiyo kwani elimu ambayo wameipata imewasaidia kufahamu namna ya kuepuka sumu kuvu katika vyakula wanavyoviandaa.

Sauti ya baadhi ya wanawake