

4 March 2025, 12:00 pm
Shirika lisilo la kiserikali la So They Can limepongezwa kwa mchango wao wa kufanya maendeleo hapa nchini hasa katika sekta ya elimu
Na Marino Kawishe
Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Daniel Silo Amesema serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wawekezaji mbali mbali ikiwemo shirika la So They Can Tanzania ili kutimiza azma ya kuleta maendelo kwa wananchi wake.
Naibu waziri Silo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijijini cha Endagile kwenye kata ya Mamire Wilayani Babati Mkoani Manyara waliojitokeza wakati akizindua madarasa na ofisi za waalimu zilizojengwa kwa ushirikiano na shirika la So They Can Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la SERIKALI la So They Can Tanzania Roselyne Mariki amesema Shirika hilo limetenga Bajet ya sh Bilion 1.7 kwajili yakutekeleza miradi mbali mbali kwenye kata nne ambazo wamekuwa wakifanya nazo kazi tangu mwaka 2018 hadi sasa.
AIDHA Roselyne amesema Shirika hilo la STC limechangia asilimia 85 kufanikisha ujenzi wa Madarasa manne na Ofisi nne za waalimu na iliyobaki ni nguvu za Wananchi.