FM Manyara

Wafanyabiashara Babati walalamika kuondolewa kwa vibanda vyao

10 January 2025, 5:12 pm

Picha ya miongoni mwa vibanda vilivyoondolewa

Wajasiriamali wanaofanya  shughuli zao katika hifadhi ya eneo la barabara kuu mjini Babati mkoani Manyara wamesema serikali ingewashirikisha na kuwapa mda wa kutafuta maeneo mengine kabla ya kuwaondoa  kwenye maeneo hayo.

Na George Agustino

Kufuatia  zoezi la kuwaondosha wajasiriamali wanaofanya shughuli zao katika hifadhi ya eneo la barabara kuu mjini Babati mkoani Manyara wajasiriamali hao wamesema serikali ingewashirikisha na kuwapa mda wa kutafuta maeneo mengine kabla ya kuwaondoa  kwenye maeneo hayo.

Wakizungumza na fm Manyara leo baadhi ya wajasiriamali hao wamesema biashara walizokuwa wanafanya kando ya barabara ndio kazi pekee wanazotegemea kuwaingiza kipato cha kujikimu kimaisha na wanapoondolewa bila kupewa muda wa kujiandaa wala kuonyeshwa eneo mbadala watashindwa hata kupeleka watoto shule  na kurejesha mikopo waliyochukua kwaajili ya biashara.

sauti ya baadhi ya wajasiriamali

Aidha, fm Manyara imezungumza na mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Shaban  Mpendu amesema taarifa za kuwaondoa wafanyabiashara hao zimetolewa mapema na utaratibu wa kuwaondoa wafanyabiashara wote kando ya barabara ni zoezi endelevu na kwa mfanyabiashara anayehitaji  eneo la kufanyia biashara anatakiwa kumfuata afisa biashara ili aelekezwe sehemu sahihi ya kufanyia biashara yake.

sauti ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Shaban  Mpendu