Mwili wa aliyefariki kwa kushindwa kulipa 150,000 ya matibabu waagwa
19 December 2024, 6:53 pm
kufuatia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Benedict Ntabagi amewasimamisha kazi watoa huduma wa tatu wa kituo cha afya cha magugu akiwemo Afisa Tabibu,Afisa Muuguzi msaidizi na Mteknolojia wadawa kwa kushindwa kutekelekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
Na Hawa Rashid
Mwili wa mwanamke aliyeng’atwa na nyoka na kufariki katika kituo cha Afya cha Magugu kwa kushindwa kulipa kiasi cha shilling 150,000 Juliana Obed umeagwa jana usiku nyumbani kwake katika kitongoji cha majengo kijiji cha Magugu wilayani Babati mkoani Manyara na kuzikwa leo Dember 19 Tarafa ya Elerai kata ya Terat mkoani Arusha.
Akizungumza kwa niaba ya familia shemeji wa marehemu Goodluck Laizer amesema wanazika leo katika makaburi ya familia mkoani Arusha ambapo ameiomba serikali ikemee kwa kina jambo hilo na wasifumbe macho kwakua watu wengi wanapoteza maaisha kutokana na uzembe unaotokea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Magugu Loya Amosi amesema anachoomba idara zote za Afya zilizopo ngazi ya kijiji hicho kila mmoja abadilike na wasifanye kazi kwa mazoea kwakua hata mvumilia mtumishi wa aina yoyote atakaye fanya uzembe,
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha magugu wamelaani tukio hilo nakusema watumishi wa kituo cha Afya cha Magugu wamekuwa wakiwanyanyasa nakutowatendea haki wanapokwenda kupata matibabu wanakuwa hawana uangalizi mzuri na badala yake wamekuwa wakifanya shughuli zao.
Aidha kufuatia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Benedict Ntabagi amewasimamisha kazi watoa huduma wa tatu wa kituo cha afya cha Magugu akiwemo Afisa tabibu,Afisa muuguzi msaidizi na Mteknolojia wadawa kwa kushindwa kutekelekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.