Afariki kwa kushindwa kulipa 150,000 ya matibabu baada ya kung’atwa na nyoka
16 December 2024, 8:51 pm
Juliana Obed mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa kitongoji cha majengo kijiji cha magugu wilayani Babati Mkoani Manyara amefariki kwa kung’atwa nyoka baada ya kushindwa kulipa kiasi cha shillingi la 150,000 kwaajili ya matibabu aliyotakiwa kulipa katika kituo cha Afya cha Magugu.
Na Hawa Rashidi
Mwanamke aliyefamika kwa jina la Juliana Obed mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa kitongoji cha majengo kijiji cha magugu wilayani Babati Mkoani Manyara amefariki kwa kung’atwa nyoka baada ya kushindwa kulipa kiasi cha shilling 150,000 kwaajili ya matibabu.
Akizungumzia tukio hilo mume wa marehemu aitwaye Obed Meiguani lazier mwenye umri wa miaka 50 amesema mkewe alin’gatwa na nyoka dec 15 2024 alipokuwa anachuma mboga ambapo alimpeleka katika kituo cha afya cha magugu lakini alishindwa kutibiwa baada ya kushindwa kulipa kiasi cha fedha amabacho aliambiwa alipe ili apatiwe matibabu hali iyomlazimu kwenda kutafuta kiasi cha shilling 130,000 lakini baada ya kuleta pesa hiyo mkewe alianza kupatiwa matibabu na alifariki baada kuchomwa sindano ya kuzuia sumu.
Kwa upande wao watoto wa marehemu Abedinega Obed na Yona Laizer wamesema kabla ya mama yao hajafariki alisema ameng’atwa na nyoka mkononi na kuonyesha mikono yake ambayo ilishaanza kuvimba baada ya sumu kuanza kusambaa nakusema waaguzi wa zahanati hiyo walitanguliza maslahi mbele badala ya utu ambapo wameiomba serikali kuchukua hatua kutokana natukio hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha magugu Loya Amosi amesema tarifa hizo amezipokea kwa mshituko asubuhi ya leo Dec 16 2024 nakulaani tuko hilo na kuahidi kuchukua hatua stahiki kutokana na mgonjwa kutokupatiwa matibabu nakusema amekwisha waliana na mganga mfawidhi wa zahanati hiyo ili kufahamu ukweli wa tukio hilo.
Aidha, Fm Manyara imemtafuta mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya cha magugu Dkt Kusta ndunguru ambaye amesema taarifa hizo amezipata akiwa safarini ambapo alipigiwa simu na mume wa marehemu akimuuliza kuhusu kiasi cha pesa alizoambiwa atoe katika hospitali hiyo na hakumwambia kama amekwamwa kuhusu kulipa pesa nakusema inawezekana kifo cha mama huyo kimepelekea kucheleweshwa kupelekwa hospital na kuahidi kufatilia tukio hilo kwa daktari aliyekuwa zamu.