Wajasiriamali Babati mji wakabidhiwa Millioni 211
20 November 2024, 12:41 pm
Vikundi 19 vya wajasiriamali wa halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara, vyakabidhi mkopo wa shilingi millioni 211 ikiwa ni lengo la serikali kuwakwamua wananchi kiuchumi.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda, amekabidhi shilingi millioni 211 ambayo ni mikopo kwa vikundi 19 vya wajasiriamali pesa ambayo ni asilimi kumi ya mapato yatokanayo na halmashauri.
Baada ya kukabidhi fedha hizo, Kaganda amewataka wajasiriamali hao kufanya biashara ambayo itawaingizia kipato ili warejeshe mikopo hiyo kwa wakati ili kuvipa fursa vikundi vingine kukopeshwa.
Amesema lengo la serikali kurudisha mikopo hiyo ni kuwainua kiuchumi vijana, wanawake na makundi maalumu ili kuongeza ajira za watu kujiajiri na sio kusubiria kuajiriwa.
Akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi, mwakilishi wa vikundi hivyo Almas Ramadhani, ameishukuru serikali kwa kurudisha mikopo hiyo na kuahidi kurejesha pesa hizo kwa wakati.
Aidha, mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shabani Mpendu amesema wana kiasi cha zaidi ya shillingi milioni miatano hamsini kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana na makundi maalum .