FM Manyara

Sendiga aikabidhi hekari 8 Tasisi ya Mwinyi Baraka Islamic Foundation 

4 November 2024, 4:59 pm

Baada ya mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga kuikabidhi hekari 8 Taasisi ya Mwinyi Baraka Foundatin amesema uwekezaji huo utaisaidia kuwainua vijana kwa kujifunza shughuli mbalimbali pamoja na kujiajiri kufuatia kuwepo kwa changamoto ya ajira kwa vijana wengi

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amekabidhi eneo la hekari 8 lililoko Makatanini wilayani Babati mkoani Manyara kwa taasisi yaMwinyi Baraka IslamicFoundation kwa ajili ya huduma za kidini ya imani ya kiislamu.

Akiongea baada ya kukabidhi eneo hilo Sendiga amesema huo ni uwekezaji mkubwa ambao umefanyika katika mkoa wa Manyara,na amewakaribisha wananchi wanaotaka kuwekeza mkoani Manyara kuwekeza kwa kuwa kuna fursa nyingi.

Amesema uwekezaji huo utaisaidia kuwainua vijana kwa kujifunza shughuli mbalimbali pamoja na kujiajiri kufuatia kuwepo kwa changamoto ya ajira kwa vijana wengi na uwekezaji huo utasaidia kupunguza ongezeko la wategemezi.

sauti ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Kwa upande wake mjumbe wa Baraza la ulamaa Taifa Shekhe Issa Othuman Issa, ameupongeza uongozi wa mkoa kwa kukubali uwekezaji huo, ambapo amesema mbali na msikiti wataweka huduma mbalimbali za kijamii.

sauti ya mjumbe wa Baraza la ulamaa Taifa Shekhe Issa Othuman Issa,

Aidha,mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda,amesema wamefurahishwa na uwekezaji huo kwakua utaleta manufa katika wilaya ya Babati mbapo mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdurahman Kololi ameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi za kidini.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdurahman Kololi