Madaktari bingwa 45 wawasili Manyara
24 September 2024, 11:15 am
Mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kagandaamewataka wananchi mkoani Manyara kutumia fursa za matibabu zinazotolewa na madaktari bingwa bobezi 45 pamoja na wataalamu wa afya 27 kutoka wizara ya afya kwa muda wa siku sita.
Na George Augustino
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kupata huduma za matibabu katika hospitali zote za halmashauri ya mkoa wa Manyara ambapo huduma hizo zinatolewa na madaktari bingwa bobezi wa magonjwa mbali mbali kutoka wizara ya afya kuanzia septemba 23 hadi septemba 27 mwaka huu
Akizungumza katika hafla ya kuwapokea madaktari hao bingwa nabobezi katika hospitali ya mji wa Babati mrara mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amewataka wananchi mkoani Manyara kutumia fursa hiyo ya matibabu ambapo huduma hiyo itatolewa kwa muda wa siku sita na madaktari 45 pamona na wataalamu wengine wa afya
kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Manyara Andrew method lyaruu amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwaleta madaktari bingwa bobezi katika mkoa wa Manyara na ameahidi kutoa ushirikiano kwa madaktari hao ili wananchi watakofika wapate huduma kwa wakati unaotakiwa.
Aidha baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma hizo wameshukuru ujio wa madaktari hao na kuiomba serikali kuendelea kutoa huduma hizo mara kwa mara katika mikoa ili kuwafikia wananchi wote kwa urahisi na kupunguza gharama za matibabu.