Wananchi Manyara wahimizwa kufanya usafi
21 September 2024, 10:51 am
Halmashauri ya mji wa Babati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Babati ili kuedelea kutunza usafi wa mazingira na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Na Mzidalfa Zaid
Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya usafi duniani september 20, halimashauri ya mji wa Babati imeadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mji ili kuuweka mji katika hali ya usafi pamoja na kupunguza magonjwa ya mlipuko.
Akiongea baada ya kushiriki zoezi hilo la usafi leo sept 21,2024 afisa afya mkoa wa Manyara Switen Mwabulambo amewataka wananchi kuendelea kufanya usafi katika mazingira yao ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko.
Kaim mkurugenzi halmashauri ya mji wa babati Florence Hundi amesema lengo la kufanya usafi ni kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuepusha serikali kutumia gharama kubwa za kutibu wananchi ambao wanaathirika na magonjwa yatokanayo na uchafu.
Kwa upande wake mwakilishi wa jeshi la polisi Lucas Mwakatundu, amesema wametii wito kutoka kwa mkurugenzi kushiriki usafi hivyo wameshiriki zoezi hilo ili kutunza mazingira ya halmashauri ya mji wa babati na kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu ya uhai hauna mbadala,zingatia usafi wa mazingira.
Nae katibu wa soko la Silent inn Sara Sospeter ameishukuru halmashauri ya mji wa Babati kwa kuliteu soko hilo kuwa miongoni mwa maeneo ambayo yamefanyiwa usafi na kuomba uongozi wa halamashauri hiyo kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara babarani na kuwapeleka kwenye soko hilo ili kuongeza wateja katika soko hilo.