FM Manyara

Wakulima watakiwa kuuza mazao stakabadhi ghalani

August 23, 2024, 5:53 pm

Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kuacha tabia ya kuuza mazao kwa walanguzi.

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi  mkoani Manyara wametakiwa kujiunga na kusajiliwa kwenye vyama vya ushirika ili kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na vyama hivyo ili wafanye kazi zao za kuuza mazao kihalali.

Wito huo umetolewa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara Absalom Cheliga wakati akiongea na FM Manyara, amesema vyama hivyo vinawasaidia pia wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao kwa pamoja na kuuza kwa bei ambayo haiwakandamizi.

Sauti ya mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Absalom Cheliga

Kwa upande wake afisa ushirika ofisi ya mrajis msaidizi mkoa wa Manyara Godamen Merinyo, amesema mazao ambayo yanakusanywa kwenye vyama vya ushirika katika mkoa wa Manyara ni pamoja na ufuta, mbaazi na dengu.

Aidha, amewataka wakulima kuhakikisha wanauza mazao yao katika stakabadhi ghalini na sio kuuza kwa walanguzi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, huku akiwataka wanunuzi kujisajili kwa soko la bidhaa Tanzania ili washiriki kwenye minada ya mazao.

Sauti ya afisa ushirika ofisi ya mrajis msaidizi mkoa wa Manyara Godamen Merinyo