Aliyebaka mwenye ulemavu ahukumiwa kwenda jela miaka 30
24 July 2024, 11:00 am
Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Babati Martin Masao amesema mnamo februari 6, 2024 Ramadhan Idd Kipusa alimbaka na kumlawiti binti wa miaka 19 ambaye ni mwenye ulemavu wakati mama mzazi wa binti huyo akiwa njiani kuelekea dukani kupeleka maandazi.
Na mzidalifa Zaid
Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imemuhukumu kwenda jela miaka 30 na kulipa fidia ya shillingi laki tano Ramadhan Idd Kipusa (19) ambaye alibaka na kumlawiti binti wa miaka 19 mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea.
Hukumu hiyo imetolewa julay 23,2024 na hakimu wa mahakama hiyo, Martini Masao ambapo amesema kipusa alitenda kosa hilo februari 6, 2024 wakati mama mzazi wa binti huyo akiwa njiani kuelekea dukani kupeleka maandazi ndipo Kipusa alipotumia mwanya huo kumbaka na kumlawiti binti huyo.
Hakimu Masao amesema mshatakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea, ambapo aliieleza mahakama hiyo kuwa hajafanya kosa hilo na mahakama imemuonea, ambapo hakimu Masao amesema mshitakiwa anaweza kukata rufaa kama hajaridhika na maamuzi yaliyotolewa mahakamani hapo.