Polisi Manyara yakamata watuhumiwa 50 wa uhalifu
18 July 2024, 2:03 pm
Jeshi la polisi mkoani Manyara limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kufichua wahalifu wa makosa ya ukatili wa kingono, dawa za kulevya na umiliki wa silaha kinyume na sheria ili mkoa uendele kuwa salama.
Na Angela Munuo
Jeshi la polisi mkoani Manyara limesema katika kipindi cha kuanzia mwezi january hadi julai 2024 wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 50 waliohusika katika matukio mbali mbali ya uhalifu ikiwemo wizi na ukatili kwa kijinsia ambapo washtakiwa 13 wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na washtakiwa 7 wamefungwa kifungo cha maisha .
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara George katabazi ameyasema hayo julay 17alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata silaha nne ambazo ni pisto mbili pamoja na magobore mawili ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria .
Kamanda Katabazi amesema jeshi la polisi katika operesheni zake wamefanikiwa kukamata pikipiki sitini na tano ( 65) zinazozaniwa ni mali ya wizi pamoja na watuhumiwa (25) wa makosa ya wizi nakusema katika kesi za ukatili wa kingono washtakiwa saba wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti na kubaka watoto wenye umri kati ya miaka 5-14 na wengine 13 wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Aidha Kamanda Katabazi amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kufichua wahalifu wa makosa ya ukatili wa kingono, dawa za kulevya na umiliki wa silaha kinyume na sheria ili mkoa uendele kuwa salama.