FM Manyara

Mzee wa miaka 78 ambaka binti mlemavu wa miaka 10

July 3, 2024, 4:25 pm

Picha ya tukio la ubakaji

Baada ya mzee wa miaka 78 kumbaka binti wa miaka kumi mwenye ulemavu wilayani Babati mkoani Manyara jeshi la polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kutokana na matukio mengi kama hayo kutokea katika mkoa wa Manyara.  

Na George Augustino

Binti mwenye umri wa miaka kumi ambaye ni mlemavu  amebakwa na mzee aliyefahamika kwa jina la Mohamed Gingi mwenywe umri wa miaka 78 akiwa nyumbani kwao wakati mama yake akiwa jikoni anapika.

Akizungumza na FM Manyara  diwani wa kata ya Kiru Keremu Benjamin Keremu amesema tukio hilo limetokea Julai1, 2024 majira ya saa tano asubuhi nyumbani anapoishi  binti huyo  na mama yake ambapo mzee huyo alikuwa amelewa.

Karemu amesema  baada ya tukio hilo wananchi walimkamata mzee huyo na kumfikisha katika kituo cha polisi na binti huyo akapelekwa katika hospital ya Mji wa Babati Mrara kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata.

Sauti ya Diwani wa kata ya Kiru

Aidha diwani huyo amewataka wananchi wa kata ya Kiru kuacha tabia za ulevi ambazo zinapelekea kufanya matukio kama hayo yasiyofaa katika jamii kwa kuwa tukio kama hilo limewahi kutokea mwaka juzi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Kiru

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi amesema ni kweli tukio hilo limetokea na jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi.

Sauti ya kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Manyara