FM Manyara

 Polisi Babati yawasaka waliohusika na mauaji ya mwizi wa bodaboda

July 2, 2024, 7:46 pm

Picha ya Kamanda wa Polisi mkoani Manyara George Katabazi

Baada ya kijana mmoja anayedaiwa kuhusika kula njama ya kuiba pikipiki kuuliwa kwa kupigwa na kuchoma moto na madereva pikipiki maarufu bodaboda wilayani Babati mkoani Manyara, wanasakwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio hilo.

Na George Augustino

 Jeshi la polisi mkoni Manyara linawasaka vijana wa Boda boda waliohusika na mauwaji ya kijana anayedaiwa kuhusika na wizi wa Boda boda kwa kumpiga na kumchoma moto hadi kufa.

Kamanda  wa polisi mkoani Manyara George Katabaziameyasema hayo leo julay 2 2024 alipokuwa akiongea na Fm Manyara,amesema tukio hilo limetokea  july mosi 2024 majira ya saa sita nanusu mchana katika mtaa wa wang’warai kata ya Babati wilaya ya Babati mkoani Manyara ambapo kijana  aliye uwawa  anadaiwa  kula njama za kuiba Boda boda ya dereva aliyemkodi.

Sauti ya Kamanda  wa polisi mkoani Manyara

Aidha,kamanda Katabazi amewataka wananchi mkoani Manyara kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake  kuwafikisha watuhumiwa katika kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe  dhidi yao ambapo amesema  jeshi hilo linaendelea na oparesheni ya  kuwakamata  watu wanaomiliki  mali  za wizi ikiwemo  boda boda.

Sauti ya Kamanda  wa polisi mkoani Manyara