FM Manyara

Jamii Manyara yatakiwa kupinga vitendo vya kikatili

28 June 2024, 4:51 pm

Picha ya Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Manyara katikati akiwa anaikiliza uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji  wa mpango jumuishi wa taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMAM ) katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Ili kupunguza vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini, wazazi mkoani Manyara wametakiwa kuwalea watoto wao na kuwapa malezi bora yatayowakinga na ukatili unaofanyika katika familia na mitandao.

Na Angel Munuo

Wazazi na walezi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili na kuwalinda ikiwemo kuwaepusha na ukatili wa kimtandao ulioshamiri katika maeneo mbali mbali nchini.

Wito huo umetokewa na katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Manyara Dominic Bwette wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji  wa mpango jumuishi wa Taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMAM ) Katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Manyara,amesema wazazi wanajukumu la kuwalea watoto wao na kuwapa malezi bora yatayowakinga na ukatili unaofanyika katika familia na katika mitandao.

Sauti ya katibu tawala msaidizi

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Mtoto kwanza Kutoka Shirika lisilokuwa la kiserekali la COSITA Agustino  Balloh amesema wazazi wamejisahau katika malezi ya watoto wao jambo ambalo linapelekea watoto kujiingiza katika makundi yasiyofaa katika jamii ikiwemo  wizi na kufanyiwa vitendi vya ukatili kama ulawiti na ubakaji

Sauti ya mradi wa Mtoto kwanza kutoka COSITA

Kwa upande wake Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi ambaye pia ni mkuu wa Dawati la jinsia na watoto wilayani Babati mkoani Manyara Willness Kimario, amesema jamii kwa  ujumla wanawajibu wakupinga na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia  vinavyotokea katika familia.

Sauti ya mkuu wa Dawati la jinsia na watoto wilayani Babati mkoani Manyara