FM Manyara

 Kamanda Katabazi azindua daraja la Mapea

June 20, 2024, 8:45 pm

Changamoto ya muda mrefu iliyokuwa inawakabili wakazi wa kijiji cha Matufa kwa kukosa daraja na wananchi kushindwa kupita katika eneo hilo ambalo lilikuwa linatumika kufanyia vitendo vya uhalifu limetatuliwa.

Na Angel Munuo

Kamanda wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi amezindua daraja la Mapea Lililopo katika Kijiji Cha matufa kata ya magugu wilayani Babati mkoani Manyara daraja ambalo aliahidi kulijenga ili kupunguza vitendo vya uhalifu na kurahisisha shughuli za kijamii kwa wananchi.

Akizindua daraja hilo  kamanda Katabazi amesema eneo hilo lilikua siyo rafiki kwa wanafunzi na wanachi wa kijiji hicho ambapo lilikuwa linakwamisha shughuli za kijamii kufanyika na magari kushindwa kupita.

Amesema ujenzi wa daraja hilo utasaida kukomesha na kutokomeza vitendo vya kikatili ambavyo vilikua vikitokea katika maeleo hayo ikiwa nipamoja na tukio la kuuwawa kikatili kwa mtoto Maria lililotokea  mwezi 2 mwaka 2024 aliyekuwa anasoma chekechea.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Manyara

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mapea Philemoni Mbogo amelipongeza jeshi la polisi mkoani Manyara Kwa kuonyesha ushirikiano kwa wanachi kwa kuwajengea daraja hilo ambalo linaunganisha vijiji jirani na kurahisisha masuala ya usafirishaji.

Sauti ya Mwenekiti wa kijiji cha Mapea

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Magugu wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuwajengea daraja hilo ambalo litaondoa changamoto ya vitendo vya kikatili vilivyokuwa vikitokea katika eneo hilo kwakua awali daraja hilo lilikua halipitiki kutoka kwa wananchi wa Kijiji kimoja kwenda kijiji  kingine.

Sauti ya wananchi wa kata ya Magugu