Ubakaji, ulawiti vyashamiri Manyara
18 June 2024, 7:25 pm
Katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto mkoani Manyara jamii yatakiwa kuwapa elimu watoto wao kwakua kufanya hivyo kutawasaidia watoto hao kupambanana na kila aina ya ukatili.
Na Marino Kawishe
Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Babati imetoa ripoti ya mwenendo wa hali ya ukatili wilayani Babati mkoani Manyara tangu Januari hadi mwezi Juni kwa mwaka 2024 ambapo vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto vinatajwa kuchukua nafasi kubwa katika jamii.
Akisoma ripoti hiyo mbele ya wananchi wa kata ya Bonga waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa ambayo yemefanyika shule ya msingi Bonga mkuu wa idara ya Maendeleo Halmashauri ya mji wa Babati Diana mchonga amesema juhudi zinahitajika ili kutokomeza vitendo hivyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati, Abdurahaman Kololii amewataka wazazi na walezi kuwapa elimu watoto wao kwakua kufanya hivyo kutawasaidia watoto hao kupambanana na kila aina ya ukatili.
Aidha, siku ya mtoto wa Africa huadhimishwa kila ifikapo june 16 nakauli mbiu ya mwaka huu 2024 inasema ‘ ELIMU JUMUISHI KWA WATOTO IZINGATIE MAARIFA , MAADILI NA STADI ZA KAZI’