Maadhimisho ya damu salama kitaifa kufanyika Manyara
13 June 2024, 5:07 pm
Zoezi la uchangiaji limeanza juni 1 2024 kwakuweka kambi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara na wananchi kuchangia damu pamoja na utoaji wa elimu ambapo kilele chake kitafanyika june 14 katika ukumbi wa CCM mkoa mkoani Manyara
Na Emmy Peter
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wananchi mkoani Manyara kuchangia damu salama kwakua zoezi hilo ni la hiyari na damu hiyo itawasaidia wenye uhitaji wakiwemo kinamama wajawazito, watoto pamoja na wanaopata ajali
Sendiga ameyasema hayo leo ofisini kwakwealipokuwa akizungumza na wandishi wa habarim kuelekea siku ya uchangiaji damu salama june 14 ambayo kitaifa inafanyika mkoani Manyara, amesema mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikoa iliyo pewa kipaombele katika kuadhimisha siku hiyo na lengo la siku hiyo ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuchangi aji damu salama.
Sendiga amesema zoezi hilo limeanza kuanzia juni 1 2024 kwakuweka kambi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara kwa wananchi kuchangia damu pamoja na utoaji wa elimu ambapo kilele chake kitafanyika june 14 katika ukumbi wa CCM mkoa mkoani Manyara ambapo wataalamu watakuwepo sehemu mbali mbali za vituo vya uchangiaji damu.
Kwaupande wake Mganga mkuu wa mkoa Dokta Damasi Kayera amesema zoezi la ukusanyaji wa damu katika mkoa wa Manyara unaendelea kuboreshwa vizuri ambapo kwa mwaka jana mkoa wa Manyara ulikusanya asilimia 75 za damu salama nakusema wananchi wanatakiwa kuchangia zaidi ya chuma 15,000 kwa mwaka.
Nae mkuu wa idara ya damu salama viwango na ubora kitaifa Dustan Haule amesema mtu anaestahili kuchangia damu awe na uzito wakuanzia kilo 50 kuendelea naasiwe na magonjwa ya kudumu kama Presha, Kisukari na Saratani
Aidha,Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya damu salama duniani kwa mwaka huu inasema ”MIAKA 20 YA UCHANGIAJI DAMU ASANTE KWA KUCHANGIA DAMU“