FM Manyara

Arusha Express yaua wa 3 Manyara

June 10, 2024, 5:05 pm

Picha ya Basi la kampuni ya Arusha Express lililopata ajali na kuuwa watu watatu katika eneo la Mogitu wilayani Hanang’ mkoani Manyara

Kamanda wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi awataka wananchi mkoani Manyara kuchukua tahadhari kwa kuangalia usalama wao pindi ajali zinapotokea kwa kuacha kusogea karibu na eneo la tukio.

Na George Augustino

Watu watatu wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya dereva wa Bus la kampuni ya Arusha Express kushindwa kulimudu gari hilo nakupelekea kugonga gari aina ya  Scania kwa  nyuma na pikipiki pamoja na gari ndogo aina ya Toyota Mistubish ikiwa imepaki pembeni kusubiria kupita.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Manyara SACP George Katabazi amesema ajali hiyo imetokea June 9 2024 usiku katika eneo la Mogitu wilayani Hangang’ mkoani Manyara nakusema walio fariki katika akili hiyo ni mwanamke mmoja  aliyekuwa katika gari ndogo aina ya Toyota Mistubish pamoja na wanaume wawili. 

Sauti ya kamanda George Katabazi

Amesema majeruhi watano wa ajali hiyo akiwemo dereva wa basi hilo wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Serekali ya Tumaini iliyopo wilayani Hanang mkoani Manyara na magari yameshaondolewa  katika Barabara kuu na shughuli za usafirishaji zinaendelea.

Aidha, kamnda Katabazi amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuangalia usalama wao pindi ajali  zinapotokea  kuacha kusogea karibu na eneo la tukio ili kuepuka matukio kama hayo ikiwemo kugongwa.

Sauti ya kamanda George Katabazi